-->

Mambo Matano (5) Ambayo Wastara Hatayasahau Maishani

Staa wa bongo movie ambaye maisha yake halisi yamekuwa yaki ‘make headlines’ kwa kiasi kikubwa, Wastara, ametaja mambo matano ambayo yamemuumiza zaidi maishani, na hatayasahau katika kipindi chote cha maisha yake

Wastara

Wastara akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, amesema jambo la kwanza kubwa ambalo hataweza kulisahau ni kuondokewa na wazazi wake wote wawili, jambo ambalo lilimuumiza sana, na kuchangia kuvuruga akili na maisha yake japo Mungu alimtia nguvu ya kuendelea kupambana katika maisha.

Jambo la pili asiloweza kusahau ni ajali aliyoipata ambayo kwa kiasi fulani ilimsababishia ulemavu na kuwa changamoto kubwa kukabiliana maisha, na la tatu ni kuondokewa na mume wake aliyempenda sana, ambaye alikuwa ni muigizaji mwenzake, Sadiki Juma maarufu kwa jina la Sajuki aliyefariki dunia mwezi Januari mwaka 2013.

Jambo la nne ni maamuzi aliyowahi kuyafanya ya kutumia vyombo vya habari kuchagisha pesa kwa ajili ya kumtibu marehemu mume wake Sajuki, kwamba jambo hilo alilazimika kulifanya kutokana na shida lakini haikuwa ridhaa ya moyo wake, hivyo lilimuathiri kwa kiasi kikubwa sana kisaikolojia, na hawezi kulisahau.

Wastara akiwa na marehemu mumewe, Sajuki

“Kukaa kwenye TV na kwenye Radio kwa ajili ya kuchangisha pesa za kumtibia mume wangu kiliniumiza, kiliniathiri sana akili yangu” Alisema Wastara.

Wastara ambaye alikuwa akitambulisha rasmi movie yake mpya, alisema jambo la tano ambalo linagonga kichwa chake mara kwa mara ni kitendo cha mashabiki wake kumchukulia tofauti na alivyo kiuhalisia

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364