-->

Mambo ya Kununua Vitu Mtandaoni ‘Yamenicost’-Shilole

Msanii wa muziki bongo asiyeisha vituko, Zuwena Mohamedi maarufu kama Shilole, ameweka wazi janga lililomkuta kwenye nguo aliyovaa ambayo imeonekana kuwaacha watu midomo wazi huku wakimcheka.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Shilole amesema nguo hiyo aliagiza mtandaoni, lakini matokeo yake ilikuja kumbadilikia baada ya kuvaa.

“Kwaweli haya mambo ya kununua vitu mitandaoni yamenicost, nguo mimi nimeiona nikaagiza ikaja, nikajaribu siku ya kwanza ikanikaa vizuri tu, siku ya sherehe nikasema nivae leo ile gauni, nikavaa na ikanikaa vizuri tu, sasa balaa likaja kadri ninavoenda na yenyewe inashuka, nikasema hili sasa balaa na nishafika kwenye sherehe, ndio hivyo”, amesema Shilole.

Kufuatia tukio hilo Shilole amepost kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa hatokuja kurudia kuagiza nguo za mitandaoni, kuepuka lililotokea.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364