-->

Rais Magufuli Amtembelea Mzee Majuto Hosptalini

Siku chache baada ya MCL Digital kumtembelea muigizaji wa filamu na maigizo Mzee Majuto na kuandika habari zake kwenye gazeti la Mwanaspoti na mitandao ya kijamii, hatimaye Rais Dk John Pombe Magufuli leo Jumatano amemtembelea muigizaji mkongwe, Mzee Majuto katika Hospitali ya Tumaini jijini Dar es Salaam anakopatiwa matibabu.

Akithibitisha habari hizo, mke wa Mzee Mjuto aitwaye Aisha Mbwana amesema ni kweli Rais Magufuli amemtembelea Mzee Majuto na kuongea nae mawili matatu kuhusiana na ugonjwa wake unaomsumbua wa tezi dume.“Ni kweli amekuja na hatukuwa na taarifa, ila tulipokuwa kwenye vipimo ndipo tukaitwa kwa ajili ya kwenda kusalimiwa, tena namshukuru sana Rais kwa kuja kumjulia afya Mzee Majuto na bado tunazidi kuomba maombi ili aweze kupona kwa haraka,” alisema Aisha.

Mzee Majuto amelazwa katika Hospitali ya Tumaini iliyopo Upanga baada ya kusumbuliwa na tezi dume na bado anaendelea kupata matibabu huku akisubiria kufanyiwa upasuaji.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364