-->

Maneno ya Lulu kwa Mama Yake ni Fundisho Tosha

Mwigizaji Lulu ameandika haya jana kwenye ukurasa wake mtandaoni, ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya mama yake mzazi.

lulu241
The pic Says all…!
Umenifundisha kujua thamani ya Mama Duniani,Umenifundisha urafiki wa kweli uko vipi,undugu WA kweli uko vipi.
Pale ambapo wote walikimbia,walikuwa kinyume Na Mimi Wewe Ndo ulisimama .
Naweza kuandika maneno Milioni lkn kiukweli hakuna namna ninayoweza kukuelezea na watu wakapata picha halisi ya ulivyo
Una mapungufu yako..Ndio sikatai .
Una mabaya yako…Ndio maana hata wewe nibinadamu sio malaika
Lakini macho yangu na moyo wangu sikutazami kama inavyokutazama dunia na watu wake….Wewe ni wangu kwa Jua au Mvua,Kufa au Kupona,kucheka au Kulia…ur always there Mama angu
Watu WA duniani washaniona sifai Kwa maneno machafu Na hata Vitendo, Dah lkn wawa unaniona kama kitu kinachozidi kuwa na thamani kila iitwapo leo.
Ombi Langu kwa Mungu aendelee kukutunza kwaajili yangu,kwaajili ya familia yetu na kila aliye karibu yetu…Nakupenda Jana,Leo,Kesho na milele.
Nilitamani niandike machache lakini nimeshindwa kujizuia?
Happy birthday Mama❤️❤️❤️

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364