-->

Wema Sepetu Amrushia kijembe Diamond!

SIMBA! Kufuatia lile sakata la jina la mnyama Simba ambapo Diamond amekuwa akijiita jina hilo siku za hivi karibuni na msanii  Mr Blue kudai kuwa alilianzisha yeye kujiita simba huku mkongwe Afande Sele akisisitiza yeye ndiyo samba dume, mastaa wengi wa hapa bongo wamekuwa  wakijiita majina ya wanyama ikiwa ni namna moja ya kuchombeza sakata hilo wakati msanii Alikiba akijiita kuwa yeye ndiyo balozi wa wanyama wote.

wemaaa

Naye staa wa Bongo Movies Wema sepetu hakuwa nyuma kwenye kuchombeza sakata hilo ambapo  kupitia ukurasa wake  wa Instagram aliandiaka;

“Watu walikuwa wanasubiria na mimi nitaje jina langu la mnyama… Mi ni Mnyama Ndio na Jina Langu ni WEMA SEPETU…. Gnyt Y’all…. Langu mwenyewe hilo…. Ila Balozi Kasema…. hihihihihi,” ameandika Wema.

Wengi memeona kuwa hilo ni dongo kwa wasanii wote wanaogombania jina la mnyama Simba akiwemo Diamond na kumsifia msanii Ali Kiba ambaye alijiita yeye ni balozi  wanyawa wote kwa kuwa yeye ni moja kati ya mabalozi wa shirika la  Wild Aid, shirika linalopigania haki za wanyama.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364