Manji Atoka Polisi kwa Gari la Wangonjwa
Dar es Salaam. Mfanyabiashara Yusuf Manji ametolewa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi muda mfupi uliopita na kupandishwa kwenye gari la wagonjwa ambalo lilipita Barabara ya Sokoine kuelekea Posta Mpya.
Mwandishi wa Mwananchi alikuwa eneo hilo ameshuhudia Manji akipanda gari hilo la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lakini hawakufahamu mara moja alikoelekea.
Manji alikuwa amevaa fulana, suruali na viatu vya wazi vyote vya rangi nyeusi.
Gazeti la Mwananchi