-->

Mapenzi Kando, Nafanya Kazi – Jacqueline Wolper

Diva wa Bongo Movie Jacqueline Wolper amesema kuwa haoni haja ya kuwa na mahusiano kwa wakati huu, japo kuwa wanaume wengi wenye pesa wamekuwa wakimsumbua kumtaka kimapenzi, na kwamba anaamini ni wasumbufu tu na hawana mapenzi ya kweli.

Wolper  amefunguka hayo karibuni na kusema kwama  kutokana na upendo wa kweli anaojitahidi kumuonyesha mwanaume anapokuwanaye kwenye uhusiano na kujikuta akiambulia maumivu, ameona bora aweke kando masuala ya mapenzi na kuwa`bize’ na kazi zake.

 “Sina mpenzi kwa sasa nimeona bora niweke pembeni haya mambo nidili na kazi zangu tu ndo muhimu, nikisema nipende hawa wanaonisumbua `now’ nitapenda sana na nitakuwa kimapenzi, lakini bado wote wanaonisumbua hakuna aliyefaulu kunishawishi niwe naye,” alisema Wolper.

Wolper kwa sasa amekanusha kuwepo kwenye mahusiano baada ya kuachana na mpenzi wake ambaye ni mwanamuziki hivi karibuni

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364