-->

Masanja Awaangukia Polisi, Wamaliza Msala wa Kuvaa sare Zao

Katika harusi ya Masanja Mkandamizaji iliyofanyika Agosti 14, wachekeshaji wenzake wa kundi la Orijino Komedi, walikuja wamevalia nguo zilizofanana na sare za jeshi la Polisi hali iliyowapelekea kukamatwa. Walifikishwa kituo cha Polisi kwa mahojiano na pia wakakaguliwa sehemu wanazoishi ili kuweza kufahamika kama kuna kitu kingine wanachomiliki tofauti na sare za Polisi.

MASANJA345

Masanja Akiwa na Monica

Kufuatia hatua hiyo, Masanja Makandamizaji ameandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Facebook kwenda kwa mashabiki wao wanaoulizia kuhusu hatma ya wachekeshaji hao waliokuwa wanashikiliwa na Polisi.

“Jamani asanteni kwa maombi yenu na meseji zenu za kuulizia juu ya ishu ya Polisi, tunamshukuru Mungu tumewaomba msamaha na wametusamehe hivyo imekwisha.

Tumesema tulinogewa na harusi tukasahau kwenda kuomba kibali. Lakini wakina Joti, Seki, Mac Reagan na Wakuvanga wamepata kautamu ka mahojiano. Ishukuriwe honeymoon imeniokoa mwee na mimi ningekuwa kwenye jiji la Makonda ingenihusu.

Hii ilikuwa karibu Monica maana alishaanza kupata presha, eti ananiuliza na wewe ukirudi utaenda Central, nikasema sio mimi tu, ni mimi na wewe”.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364