Masanja: Nimenunua BMW X6 Kama Mtu Mwingine Anavyonunua Baiskeli
Mchekeshaji wa Orijino Komedi na mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji amesema kila anachomiliki amekinunua kwa pesa yake halali huku akishangaa kwanini watu wameshtuka baada ya kuona anamiliki BMW yenye plate namba ya jina lake.
Akizungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Ijumaa hii, Masanja alisema anamiliki magari mengi huku akidai BMW X6 ameinunua kama mtu mwingine anavyonunua baiskeli.
“Mimi nina magari mengi sana na yote nayachukulia kama chombo cha usafiri cha kunitoa point moja kwenda nyingine,” alisema. “Sasa nashangaa watu wanaongea sana kuhusu mimi kwani gari kitu gani! Hiyo BMW X6 nimenunua kama watu wengine wanavyonunua baiskeli,” alijinadi.
Aliongeza, “Na hata hao TRA kama wananisikia waje hapa Clouds nimekuja nayo ipo hapo chini ili waangalie kama sijailipia.”
Masanja alisema anafanya biashara za aina mbalimbali hivyo kununua gari la thamani siku kitu cha ajabu kwakuwa anaweza kununua kupitia biashara yake moja tu.