-->

Mastaa Tunajimaliza Wenyewe- Johari

BLANDINA Chagula ‘Johari’ amefunguka kwa kuwachana waigizaji wezake nyota kuwa wanajisahau na kushindwa kuhamasisha wadau kuipa thamani kazi yao ya filamu na kuwa watu wa kutumika tu katika shughuli ambazo hazielezei fani yao na kuwa gumzo kwa jamii.

Akiongea na FC Johari amesema ameshangazwa na wasanii nyota kuwa nyuma katika shunguli ambazo ni kwa ajili ya kazi zao na wamekuwa mahiri kuhudhuria shughuli ambazo hawana hata maslahi nazo, pia msanii huyo alitumia fursa hiyo kuwapongeza waandaaji wa Bongo Movie Night kwa kuwakumbuka.

“Si siri tasnia yetu tunaiua wenyewe kwa kuendekeza ustaa ambao pengine mashabiki zetu hawatuelewi, leo ni siku muhimu katika usiku wa Bongo Movie Night inatakiwa tuwe wengi kuonana mashabiki zetu,”alisema Johari.

Johari alisema hayo akiwa katika onyesho la filamu za kibongo la Bongo Movie Night ambalo linafanyika kila alhamisi ya mwisho wa mwezi na filamu ya Johari ndio ilionyeshwa, Johari anasema kuwa wapenzi wa kazi zao wengi wapo mtaani hawapatikani Mlimani City wala sehemu za kifahari bali wapo Manzese, Tandika nk.

Kwa kuliona hilo Filamucentral kwa kushirikiana na Production X wanakuletea sinema mtaani kwako kupitia Sinemani kila sehemu yenye sehemu ya kuonyeshea sinema wataangalia filamu kila siku.

FilamuCentral

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364