-->

Mboto na Riyama Wamshushua Tunda Man

Mchekeshaji maarufu hapa nchini, Mboto, pamoja na muigizaji wa filamu Bongo movies, Riyama Ally, wamekanusha kufanya filamu ya ‘Mama Kijacho’ kama alivyodai mwanamuziki Tunda Man ambaye ndiyo alijinadi kuwa muhusika mkuu.

riyama2300

Mboto amekanusha hayo mbele za kamera ya eNewz na kusema kuwa “mimi sijawahi kushuti movie ya mama kijacho,” alisema Mboto alizidi kuongeza kuwa “Msema kweli mpenzi wa Mungu, Hata Mzee Magufuli anakwambia hivyo hivyo yule msema kweli mpenzi wa Mungu”.

eNewz iliamua pia kuweka sawa kwa kuwasiliana na Riyama Ally ambaye alikuwa yupo nchini Kenya kwa ajili ya kufanya filamu nyingine nchini huko, naye alikanusha kufanya filamu ya Mama Kijacho na Tunda Man kama ilivyo kwa Mboto.

Majuma machache yaliyo pita, Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Man alifanya mahojiano na eNewz ambapo alisema kuwa wapo kambini waigizaji mbali mbali akiwemo Mboto na Riyama Ally.

eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364