Meneja wa Wema Afungukia Ugomvi wa Mirror na Petiti Man
Mwanamitindo na Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amefunguka juu ya ugomvi wa Mirror na Petiti Man.
“Petiti bado yupo Endles Fame kwakuwa bado hajaiandikia barua kampuni kuwa anatoka na yote yaliyotokea kati ya petit na Mirror ama Wema ni tofauti zao tu kawaida ambazo si mara ya kwanza kutokea”,alisema Kadinda.
Hapo awali Mirror aliiambia Enewz kua hasimamiwi tena na Petit katika kazi zake huku Petit akitaka tumuulize Meneja wa kampuni ambaye ni Kadinda juu ya swala hilo kwakuwa yeye ndo msemaji wa kampuni hiyo.
eatv.tv