Mbu mwenyewe anaweza kuondoa malaria
Mbu mwenyewe anaweza kuja ondoa malaria. Je, ni kweli? Tafiti ndio zinasema, endelea hapa chini
Kila mwaka, watu bilioni 3.2 wako katika hatari ya kuamukizwa malaria kutoka kwa mbu walioambukizwa na vijidudu vinavyosababishwa malaria. Lakini labda si kwa muda mrefu tukajasikia malaria imefutika kabisa.
Sio ajabu tukasikia mtu anasema hii itakuwa ni uongo,ndoto au haitawezekani kabisaaaa. Mwaka jana, 2015 wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha California walifanya utafiti na kufanikiwa kupata njia mbadala ya kupambana na ugonjwa huo kwa kutumia DNA ya Mbu mwenyewe.
Kivipi au jinsi gani?
Watafiti watatu, waliojulikana kama Anthony James, Ethan Bier na Valentino Gantz waliungana kwenye tafiti hiyo kwa kuhariri jeni (genes) za mbu mwenyewe kwa kutumia zana mpya iliyojulikana kwa jina la kitaalamu la kiingereza kama CRISPR (“Clustered Regularly Interspaced Short Palindromic Repeats“). Tafiti walichofanya hawa wataalamu ilikuwa ni kubadilisha chembechembe hizo, kwa kuuwa vimelea vinavyosababisha malaria na kupandikizwa vimelea vingine visivyokuwa vinasababisha malaria. Mbu atakayepandikizwa hivi vimelea (jeni) ataweza kuzaa mbu ambaye atakuwa na jeni (genes) zinazo pambana na malaria. Jeni (Gene) hizi itaenea kwa mbu mmoja hadi mwingine na mwishowe mbu wote wataozaliana watakuwa hawawezi tena kusababisha malaria baada ya mbu wote kuwa na genes mpya.
Kwa hiyo mtu yeyote atakaye ng’atwa na mbu mwenye jeni (genes) hizi mpya hatapata tena malaria. Kwa wale wanaojua kimombon basi bofya hapa