Miss Tanzania Afunguka Haya Kuhusu Alikiba
Miss Tanzania 2016, Diana Edward amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye anampenda sana Ally Saleh alimaarufu kama ‘Ali Kiba’ kutokana na ukweli kwamba msanii huyo amejiweka tofauti na wasanii wengine na ametulia.
Miss Tanzania ameweka wazi hilo kupitia kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio wakati akipiga stori na Big Chawa na kusema yeye anamkubali sana Alikiba kutokana na ukweli kwamba ametulia ukilinganisha na wasanii wengine wa kiume bongo.
“Tatizo Watanzania mabigwa wa kubadili vitu ukisema hivi wao wanabadili vingine lakini msanii wa kiume ninayempenda Tanzania ni Alikiba, nampenda kwa kuwa nadhani ametulia najua wengine nao wametulia ila mimi namuongelea yeye kuwa ametulia na mambo yake haweki wazi kama wengine hivyo mimi namuona ametulia ndiyo maana nampenda’ alisisitiza Diana