-->

Idriss Afunguka Kumpa Mimba Wema Sepetu

Muigizaji wa filamu na mchekeshaji mahiri katika masuala ya komedi Idris Sultan amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli alifanikiwa kumpatia ujauzito Wema Sepetu tena wa watoto wawili lakini kwa bahati mbaya uliharibika.

Idris Sultan amesema hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni. Moja ya shabiki alitaka kufahamu kama kweli alimpa ujauzito Wema Sepetu ndipo hapo aliposema ni kweli.

“Wema Sepetu kweli nilimpa mimba na ni kweli kwamba ilikuwa ni mimba ya watoto mapacha, hivyo haikuwa kiki na kweli nilikuwa kwenye mahusiano naye kwa takribani miaka miwili hivyo haikuwa kiki ile bali uhalisia” alisema Idris Sultan

Mbali na hilo Idris Sultan amedai baadaye aliamua kumuacha mwanadada huyo kutokana na mambo mbalimbali ambayo alimtendea na kuamua kusonga mbele na maisha yake binafsi

“Tangu nimekuwa maarufu sijawahi kuachwa, kabla ya umaarufu nimeachwa mara tatu, kwenye mahusiano huwaga sisemi ‘its over’, hivyo nilimuacha Wema Sepetu ila kwanini niliachana naye siwezi kuweka wazi, kufanya hivyo nitakuwa namkosea maana naweza kuweka mambo hadharani kumbe kuna mwanaume mwingine anamtaka saizi nitakuwa simtendei haki ila nachoweza kusema nilimuacha kwa sababu ya vitu alivyofanya kwangu” alisisitiza Idris Sultan

source:udakuspecially

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364