-->

Mititu Aelezea Jinsi Marehemu Edwin Semzaba wa ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’ Alivyogusa Maisha Yake ya Sanaa

MTITU45
Kufuatia kifo cha mwandishi wa vitabu vya Kiswahili kikiwemo, Ngoswe: Penzi Kitovu cha Uzembe, Edwin Semzaba amefariki dunia jana Jumapili ya January, 17, muongozaji na mtengenezaji wa filamu maarufu hapa bongo, Willium Mtitu kupitia ukurasa wake mtandaoni alieza jinsi alivyoguswa na msiba huo.

Pumzika kwa amani mwalim mimi ni mmoja kati ya watu aliyefamikiwa kuongoza(KUDIRECT)mchezo kuigiza unaotoka na kitabu chake cha NGOSWE: PENZI KITOVU CHA UZEMBE ambao ulichezwa na wanafunzi wa shule ya secondary ya ST PETERS iliyopo kimara .project hiyo ilikuwa chini ya kituo cha TANZANIA THEATER CENTER (TZTC) Chini ya marehemu Edwin Kaduma.
kiukweli kitabu hicho kina mafundisho makubwa sana juu kuhusu kuchanganya kazi na mapenzi tutakukumbuka daiama mwalim mbele yako nyuma yetu bwana ametoa bwana ametwaa.

 

Marehemu Edwin alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM kwenye idara ya sanaa za maonesho. Semzaba anakumbukwa kwa uandishi wake mahiri hususan kwa kitabu cha mchezo wa Ngoswe; Penzi Kitovu cha Uzembe kilichotumika kwenye shule za sekondari katika somo la Kiswahili.

Baadhi ya vitabu vya hadithi alivyoandika ni pamoja na Marimba ya Majaliwa, 2008, Funke Bugebuge, 1999, Tausi wa Alfajiri, 1996 na Tamaa ya Boimandaa, 2002

Michezo aliyoiandika ni pamoja na Kinyamkera, 2014, Joseph na Josephine, , 2014, Mkokoteni, 2014, Tendehogo na Sofia wa Gongolambotoa 1985.

R.I.P

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364