-->

Mobeto: Sitaki Kufuata Maneno ya Mtandaoni

MWANAMITINDO, Hamisa Mobeto ameibuka na kusema kuwa hataki kuyafuata maneno ya mtandaoni kwani yanaweza kumkondesha hivyo ameamua kuyatupilia mbali.

Akiongea na Risasi Jumamosi, Hamisa alisema kuwa ili maisha yake yamuendee vizuri ameamua kutojali maneno ya mtandaoni kwani akiyaendekeza anaweza kujikuta anabaki mifupa na kushindwa kufanya mambo yake muhimu.

“Mitandaoni kunasemwa mambo mengi na kila kukicha naandikwa tu nikisema nikomae na maneno nitashindwa kufanya mambo yangu muhimu, sitaki kabisa kufuatilia na wala sijali kabisa,” alisema Mobeto.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364