-->

“Muziki wa Bongo Fleva ni bigijii”-Patcho Mwamba.

Mwanamuziki wa miondoko ya dance hapa nchini Patcho Mwamba amesema muziki wa bongo fleva hauna tofauti na bigjii maana haudumu kwa muda mrefu.

pacho

Patcho ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha E NEWS kinachorushwa na kituo cha EATV.

Patcho amesema pamoja na waandaaji wa vipindi vya redio na runinga kuwapendelea wanamuziki wa bongo fleva lakini nyimbo zao hazidumu kwa muda hata wa miezi 3.

Wasanii wa bongo fleva wanapendelewa kwenye vituo vya habari ila muziki wa dance unapigwa kwa nusu saa tena mwishoni mwa wiki lakini nyimbo zetu zinadumu kuliko wao.

Msanii huyo amewataka waandaaji wa vipindi vya muziki nchini kuacha upendeleo na kuhakikisha wanapiga nyimbo kwa usawa katika vipindi vyao.

Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364