-->

Mwili wa Mbunge wa Chadema Wawasili -VIDEO

Dar es Salaam.Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson leo Alhamisi ameongoza mapokezi ya mwili Mbunge wa viti maalumu (Chadema) Dk Elly Macha.

Dk Macha alifariki dunia Machi 31 mwaka huu katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza alikokuwa akitibiwa.

Baadhi ya viongozi waliokuwepo wakati mwili huo ukiwasili, ni mke wa Spika mstaafu Mama Magreth Sitta, mbunge wa Iringa mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa,Katibu Mkuu (UWT) Amina Makilage na Grace Tendega katibu mkuu (Bawacha).

Naibu spika, Dk Tulia amesema Bunge lilipata taarifa za ugonjwa wa marehemu ndani ya miezi mitatu na baadae kupata taarifa za ghafla juu ya kifo chake.

Alisema licha ya ulemavu wake Dk Macha alipigania haki za walemavu.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364