Mzee Zorro Alinifundisha Vitu Hivi Tangu Utotoni- Banana Zorro
Msanii mkongwe kwenye muziki wa Bongo Fleva,Banana Zorro amesema kuwa ameamua kufanya kitu ambacho amekuwa akifundishwa tangu utotoni kupitia kwa mzee wake Zahir Ally Zorro ambaye pia ni mwanamuziki wa siku nyingi,amezungumza hayo kwenye kipindi cha Power Break Fast jana.
“Kwangu mimi ilikuwa tofauti, niliamua kufanya kitu ambacho nimekuwa nikifundishwa tangu utotoni kupitia Mzee wangu, nikaja kujifunza ukubwani kupitia band tofauti kama InAfrika Band, hivyo nilipowiva nikaamua kuanzisha ya kwangu, nilichukua uamuzi wa kuifanya hii kitu na nashukuru mpaka leo naendelea kuwa hapa na B-Band.”Alisema Banana Zorro.
cloudsfm.com