Q Chiller Adondokea kwa Diamond Platnumz
MKALI wa wimbo wa ‘Mkungu wa Ndizi’ aliyerudi kwa kasi katika muziki wa Bongo Fleva, Abubakari Shaaban maarufu Q Chiller, amesema kwa sasa anatamani kufanyakazi na Diamond Platnumz.
Q Chiller alifafanua kwamba anatamani kufanya kazi na Diamond kwa kuwa wote wana uongozi unaojua kazi zao lakini anajipanga kwanza kwa kuandaa wimbo mzuri utakaowawezesha kurudisha fedha zao kupitia mialiko mbalimbali ndani na nje ya nchi.
“Najipanga kurekodi wimbo na Diamond, naamini wimbo huo utaishi na tutatengeneza fedha za kutosha nitamweleza cha kufanya ili wimbo huo usiwe mwepesi maana tunatakiwa tutoe wimbo utakaokuwa mfano wa kuigwa na wasanii wengine,” alieleza Q Chillar.
Aliongeza kwamba licha ya kuwa maarufu pia yeye ni shabiki wa msanii huyo ndiyo maana anatamani kufanya naye wimbo kutokana na uwezo alionao wa kubadilika badilika unaomsaidia kurekodi muziki bora akitolea mfano wimbo wa ‘Sing’ alioimba na AKA wa Afrika Kusini.
Mtanzania