-->

Mzungu Kichaa Awadiss Wema na Idriss

Staa wa muziki Mzungu Kichaa, amevunja ukimya kuligusia suala ambalo pengine linawaumiza wasanii wengi, ikionekana kuwa ni ‘diss’ pia kwa staa Wema Sepetu na mwenzake Idriss Sultan, kupitia suala lao la ujauzito kunasa na kutoka.

Mzungu_Kichaa

Akiongea kwa hisia nzito, Mzungu Kichaa ambaye ana project kubwa ya video ambayo watu hawaifahamu kama wanavyofahamu mimba ya Wema, msanii huyo anayejinadi kuwa ni mbishi, ameelezea kusikitishwa kwake kwa mastaa hao ambao wanatumia muda wao mwingi kuleta atensheni kwa mashabiki badala kufanya shughuli zao binafsi za kila siku.

Mzungu Kichaa pia amekanusha suala la video yake kukosa kiki kutokana na kumhusisha Dir Adam Juma ndani yake, na kuifanyia hapa hapa nchini akisema kuwa Dir Adam ana kila sababu ya kupewa hashima yake kutokana na ubora wa kazi zake na si maelezo mengine yaliyopotofu.

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364