-->

Ray : ‘Tajiri Mfupi’ Imegharimu Milioni 17

Msanii mkongwe wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ amesema filamu yake mpya ‘Tajiri Mfupu’ imegharimu milioni 17 mpaka inaingia sokoni.
Ray Kigosi

Akizungumza katika kipindi cha Clouds 360 Ijumaa hii, Ray alisema bajeti ya milioni 10 ndio bajeti kubwa kwa filamu nyingi za bongo.

“Filamu zetu nyingi za bongo kwa sisi wasanii wakubwa ni kuanzia milioni 10 hadi 20 ndio filamu inakamilika, kama mimi filamu zangu zote ni kuanzia milioni 10 na kuendelea. Kwa hii filamu yangu ya Tajiri Mfupi imegharimu milioni 17, kwa sababu RJ Company ikishakuita kama artist uje ofisini kwangu na ukishaingia utahitaji pesa kubwa, tofauti kwenye kampuni nyingine,” alisema Ray.

Pia Ray alisema moja ya sababu inayowafanya wasanii wa filamu kufanya filamu zilizo chini ya kiwango ni ufinyu wa bajeti.

Bongo 5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364