Nahitaji Demu Mzuri Anagonga Ngeri Sana- Idris Sultan
IDRIS Sultan mwigizaji na mchekeshaji katika tasnia ya filamu Bongo amefunguka kwa kusema kuwa anahitaji mwanamke ambaye atamuoa, sifa ya kwanza awe mzuri sana awe na tabia nzuri hasa ya kuwapenda watoto kwani yeye anapenda Watoto zaidi.
“Siku hizi mambo ya kidigitali mambo yanakuwa wazi tu, binafsi nampenda mwanamke mwenye sifa hizi awe na akili, ajue kuongea Kiingereza vizuri, mrembo nataka kuzaa watoto wazuri na apende watoto,”alisema Idris,
Idris anadai kuwa ataoa mwanamke anayependa watoto ili aweze kulea watoto hasa wale wanaoishi katika mazingira magumu wengi wanaishi bila kuwa na uhakika wa chakula wala sehemu ya kuishi yeye angependa kuwasaidia, Idris alipotoka katika Jumba la Big Brother akiwa na kitita cha mkwanja alikutana na Madame Wema.
Filamu Central