-->

Najuta Kuachana na Mke Wangu wa kwanza – Gardiner

Mtangazaji wa Clouds FM, Gardiner G Habash amesema miongoni mwa vitu anavyojutia katika maisha yake ni kuachana na mke wa kwanza aliyezaa naye mtoto wa kike, Karen, ambaye kwa sasa yupo mwaka wa pili chuoni.

GARDNER43

 

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gardiner alisema kutokana na kubadilisha kazi ya awali na kuwa mfanyabiashara kipindi anaishi Mwanza, alijikuta akiiweka kwenye mawe ndoa yake kwa kukosa muda nayo.

“Yale mazingira niliyokutana nayo Mwanza ya kibiashara yalisababisha nikaachana na mke wangu wa kwanza, ni kitu ambacho najuta,”alisema staa huyo. “Nisije nikasema sana mwisho nikalia hapa bure,” alisisitiza.

Amesema mke wake huyo kwa sasa aliolewa japo wana mawasiliano mazuri sababu ya mtoto wao. Kuhusu kama anajuta kuachana na Lady Jaydee, Gardiner alisema: Siwezi kusema najuta kwamba alitokea kwenye maisha yangu na siwezi kusema kwamba najuta tuliachana. Lakini ninachoweza kusema tu kwamba kwa suala la Jaydee ni suala ambalo nilichagua sana lisiwe ni jambo ambalo nalizungumzia au kulitolea comment kwasababu yule ni public figure unaposema kitu kuhusu yeye tafsiri zinakuwa ni tofauti na vile unavyotarajia.”

“Kwahiyo sina majuto yoyote, na sina aina yoyote ya chuki au uadui na nategemea hata yeye atakuwa anafeel the same,” alisisitiza.

Alidai kuwa yeye na Lady Jaydee hawana mawasiliano ya aina yoyote kwa sasa na mara ya mwisho walikutana kipindi wanakamilisha taratibu za talaka.

Kwa upande mwingine Gardiner amedai kuwa maisha aliyonayo sasa ni ya furaha tele. Mtangazaji huyo amejiunga tena na Clouds FM akitokea EFM.

Bongo5

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364