-->

Kipini Puani kwa Diamond Chazua Gumzo Mtandaoni

MFALME wa Bongo Fleva nchini anayekimbiza na ngoma yake ya Make Me Sing, Diamond Platnumz amejikuta kwenye wakati mgumu huku akishambuliwa kwa maneno kwenye mtandao wa Instagram baada ya jana Jumatano kuweka picha iliyomwonesha akiwa amevaa hereni.

diamond82

Picha hiyo ilizua sintofahamu kwa mashabiki zake huku wengi wao wakihoji imekuwaje na nini kimemsibu staa huyo kutoboa pua na kuvaa hereni. Ikumbukwe kuna wimbo wa Muziki Gani ambao Nay wa Mitego alimshirikisha Diamond na ndani yake kuna maneno ambayo Diamond ameimba ‘kuwaponda’ wasanii wa hip hop kwamba kazi yao ni kutoboa pua. Kipande cha msitari “kazi yenu kutoboa pua”.

Wewe umelionaje hili?.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364