-->

Nandy amfungukia Ruby

Msanii wa muziki wa kike hapa bongo ambaye hivi sasa ndio gumzo kwenye game, Nandy, amesema kitendo cha Ruby kusema kuwa kwake kimya alikuwa anampisha, alikuwa ana tafuta kisingizio kwani bado alikuwepo kwenye game.

Akizungumza kwenye 5SELEKT ya East Africa Television, Nandy amesema kwa Ruby kusema hivyo ni kisingizio, kwani wakati yeye anaanza kufanya vizuri, Ruby alikuwa ana kazi alizoachia baada ya kugombana na uongozi wake wa awali.

“Sio kweli kwa sababu nakumbuka wakati ambapo amegombana na uongozi wake, ana nyimbo tatu alizotoa, siamini kitu kama hicho, hapo alikuwa amepumzika au, ni kitu ambacho sio cha kweli, watu wengi wanajua Ruby alikuwa amegombana na uongozi wake na ndio akatoa hizo nyimbo, kwa hiyo kikawa kama kisingizio, alikuwa anatafuta kisingizio”, amesema Nandy.

Wasanii hao wawili inasemekana hawana maelewano mazuri tangu watu waibue hisia kwamba Nandy amekuja kuchukua nafasi ya Ruby kwenye uongozi wake wa awali, ambao ndio ulimuweka juu kwenye game

Comments

comments

Post Tagged with ,

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364