-->

Naonyesha Mali Zangu Kuwapa Nguvu Vijana-Nay

Msanii Nay wa Mitego amesema mara nyingi yeye hupenda kuonesha vitu anavyo miliki zikiwepo gari, nyumba hata pesa kwa lengo kuu moja, anadai anafanya hivyo ili kuwatia moyo vijana ambao wamekata tamaa.

Msanii Nay wa Mitego

Msanii Nay wa Mitego

Amesema anafanya hivyo kwa kuwa yeye mwenyewe alitoka katika maisha magumu ambayo alikuwa hadhani kama angeweza kufikia mafanikio hayo lakini alipambana na kupigania mpka ameweza kutoboza.

Akizungumza na eNEWS Nay wa Mitego amedai kuwa yeye si muigizaji hivyo hawezi kuwaonesha watu vitu ambavyo si vyake wala havimiliki kwani anadai kufanya hivyo anataka jamii, ndugu hata watoto wake wafahamu kuwa ana vitu hivyo ili hata siku akitokea amefariki ndugu na watoto wanakuwa wanatambua nilikuwa na vitu gani.

“Unajua mimi nilitoka kwenye maisha magumu sana, Nay nilikuwa naokota makopo, vyuma, nilikuwa mkabaji lakini nilikomaa na kutafuta maisha mpaka sasa nina maisha yangu, na familia inakula vizuri, watoto wanasoma shule nzuri napata nachotaka mimi kwa wakati, hivyo mimi kuonesha mali zangu nataka vijana wenzangu ambao wapo mtaani wasikate tamaa bali wazidi kupambana kwani wanaweza kutoboza kama watakuwa na nia na kupambana kweli” Nay wa Mitego.

“Unajua kwenye muziki kuna vijana wengi wanatamani kutoka kimaisha hivyo wanapoona mtu kama mimi nimefanikiwa ni kama nawatia hasira ya kuzidi kukomaa na kufanya kazi zaidi ili wafanikiwe zaidi na si ushamba au kujionesha bali nifanya hivyo kuwatia moyo kuwa inawezekana kama utakaza” aliongezea Nay wa Mitego.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364