-->

Nilipenda Sana Ugomvi Utotoni-Riyama

Staa wa filamu nchini, Riyama Ally amesema wakati akiwa mdogo alikuwa anapenda sana ugomvi. Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti Alhamisi hii, Riyama alisema wakati huo watu mtaani kwao walikuwa wanamuogopa.

riyama789

“Utotoni nilipenda sana ugomvi, yaani mtu asinichokoze ninaye huyo yaani nilikuwa napenda kupigana na kuingilia ugomvi hata kama haunihusu kiasi mtaani walikuwa wananiogopa, kitu ambacho nikikumbuka huwa najicheka mwenyewe,” anasema

Katika hatua nyingine muigizaji huyo amesema hakuwahi kufikiria kama angekuja kuwa muigizaji, kwani alikuwa anapenda sana kuimba taarab.

“Sio siri sikuwahi kuota kama ningekuwa kuwa mwigizaji, nilitamani sana kuwa muimbaji wa taarabu, muziki ninaoupenda mpaka leo,” anasema Riyama.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364