Nape Azungumza Chini ya Ulinzi wa Polisi
Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amezungumza na wanahabari nje ya hoteli ya Protea baada ya mkutano wake kuzuiwa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni.
Katika mkutano huo, Nape alionyeshwa kushangazwa na kitendo cha polisi kumnyooshea bunduki alipokuwa akitaka kuzungumza na wanahabari katika eneo hilo.
“Mimi ni mtu mdogo sana ndani ya Tanzania, Nape hawezi kuwa mkubwa kuliko Tanzania,” alisema Nape
Nape alisema hana kinyongo na uamuzi wa Rais John Magufuli kumtoa katika nafasi hiyo na amewaomba wanahabari kumpa ushirikiano Waziri mpya, Harrison Mwakyembe.
Nape ameondoka katika eneo hilo baada ya gari lake kuzuiwa na polisi na amewaambia waandishi wa habari kuwa atawajulisha lolote litakalotokea.