-->

Naweza Kuuza Movie Zangu Bila Kumtegemea Mhindi-Gabo

Msanii wa filamu aliyetamba kwenye Bado Natafuta, Gabo Zigamba amesema filamu yake mpya ‘Safari ya Gwalu’ aliyoisambaza mwenyewe kupitia kampuni yake ya D Entertainment, imemfanya agundue kuwa kusambaza mwenyewe filamu kuna manufaa zaidi kuliko kupeleka kwenye makampuni binafsi ya usambazaji.

Gabo akiwa na baadhi ya mashabiki wake

Gabo ameiambia Bongo5 kuwa mpaka sasa tayari filamu yake imeshasambazwa Tanzania nzima na ameuza nakala nyingi kuliko kawaida.

“Hii kazi nilitaka kuiuza tofauti yaani kujaribu kuiuza kupitia kampuni yangu,lakini matokeo niliyopata yamenifanya niamini kumbe inawezekana kufanya hii biashara pasipo kutegemea kampuni ya mtu,” alisema.

“Nimeshauza copy nyingi sana mpaka sasa na bado soko linahitaji kazi. Pia muamko umekuwa mkubwa zaidi kwa sababu Safari ya Gwalu imekuwa gumzo sana kila sehemu ninakopita. Kwahiyo naweza kusema hii kazi pamoja na njia yangu mpya ya usambazaji imenifanya nione kumbe naweza kusambaza filamu zangu mwenyewe na nikanufaika zaidi.”

Gabo ni mmoja ya wasanii wa kiume wanaotabiriwa kuja kufanya mambo makubwa katika tasnia ya filamu baada ya Kanumba.

Chanzo:Bongo5

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364