-->

Ni Bora Nitoke na Msukuma Mkokoteni – Ray C

Mwanamuziki ambaye alijipatia umaarufu kutokana na uchezaji wake na kupewa jina la kiuno bila mfupa Ray C amefungukana na kusema kwa sasa hataki kabisa kutoka kimapenzi na msanii yoyote au mtu maarufu.

ray c33

Ray C amesema hayo kupitia kipindi cha eNews na kusema toka ameachana na msanii Lord Eyes hajawahi kuingia tena kwenye mahusiano na kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana mpaka yeye kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kipindi hicho.

“Kwa sasa bado sina boy friend, now nina marafiki tu kiukweli nafasi hiyo bado maana Lord Eyes aliniumiza sana, nilimpenda sana na ndiyo maana nilifanya alichokuwa akifanya, sikutegemea kama ingekuwa vile, hata kwenye drugs unakutana na rafiki yako anafanya hiki na wewe utataka kufanya ili aone upo naye pamoja, ila kwa sasa mimi na wasanii hapana, ni bora hata nitoke na msukuma mkokoteni ili mradi anipende maana mimi nina mapenzi ya kweli ndiyo maana unaona hata nyimbo zangu nyingi ni za mapenzi” Alisema Ray C.

Ray C amekuwa akijutia sana suala la mapenzi na kukiri wazi kuwa hilo ndiyo jambo lililompelekea kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa kipindi cha nyuma kabla ya kuanzishiwa dozi kwa ajili ya kuachana na dawa hizo.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364