-->

Niliamua Kukaa Kimya kwa Malengo- Lady Jaydee

Msanii wa Bongo Fleva nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jay dee amesema yeye kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa wimbo siyo kwamba alifulia bali aliamua kutotoa wimbo kwa malengo.

LADYJAYDEE

Jaydee ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusiana na yeye kukaa muda mrefu kabla ya juzi kuachia ngoma mpya aliyoipa jina la ‘Ndi Ndi Ndi’

”Kupotea ni tofauti na mtu aliyelala na kuamka, mimi nime ‘maintain’ niliamua kutotoa wimbo na niliposema naamka tena watu walidhani ndiyo jina la wimbo lakini haikuwa malengo hayo”-Amesema Jaydee.

Aidha Msanii huyo amesisitiza kuwa kutoa wimbo siyo tuu kutoa kwa sababu watu wanatoa bali msanii anatakiwa kutumia akili na kutokurupuka katika kutoa wimbo.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364