-->

Ningemtaja Anayeniuzia Madawa ya Kulevya – Madee

Msanii wa muziki wa kizazi Kipya Madee amesema wao kama wasanii wamekuwa wakijitahidi kufanya harakati za kupambana na madawa ya kulevya, lakini serikali imekuwa haiwaungi mkono kwa kiasi kikubwa na kuwapelekea kukwama

MADEE344

Madee ameyasema hayo alipokuwa akiongea na East Africa Television, na kusema kuwa wao kama wasanii pekee hawana uwezo wa kupambana moja kwa moja, bila msaada wa serikali ambayo ndio ina nguvu kubwa ya kupambana nao.

“Nakumbuka miaka miwili au mitatu nyuma, hili suala lilishamiri kwenye muziki wa bongo fleva, nakumbuka mwanamuziki Kalapina alitoaga nyimbo inaitwa hip hop bila madawa inawezekana, na kweli zile harakati zake zilifanywa, hata sisi wanamuziki wenzake tulikuwa tupo tayari kusapoti kwa sababu tulikuwa tunapost, tunawasikilizisha mateja, so serikali ilitakiwa sasa iunge mkono, serikali ina mkono mrefu sana na ndio ina jicho kubwa sana kuliko jicho la msanii, serikali inawajua hawa watu inaweza wakawafuatilia wakakuta na ushahidi wakawafunga hawa watu”, alisema Madee.

Pia Madee amesema laiti yeye angekuwa mmoja wa wanaotumia angekuwa tayari kuwataja wanaomuuzia, ili sheria ichukue mkondo wake na kuokoa wengine.

“Nikiwa mimi natumia madawa na tayari yameshaanza kuniathiri si utaulizwa imekuwaje kuwaje, nani amekufundisha hizi mambo, umeanza wapi umenunua kwa nani, ina maana nitaanza kumtaja yule ambaye ameniuzia, na ambaye ameniuzia mimi kikete ye atamtaja bosi wake, bosi wake atamtaja yule bosi wake mkubwa kwa hiyo ile cheni yote itakuja mpaka itamfikia yule kigogo anayeingiza kutoka nje”, alisema Madee.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364