-->

Nilimpenda Jackie Cliff Ila Sitarudiana Nae-Jux

Msanii Jux ambaye kwa sasa yupo kimahusiano na Vanessa Mdee, amefunguka na kuweka wazi sakata ambalo lilimkuta mpenzi wake wa zamani anayefahamika kama Jackie Cliff na mahusiano yake na model huyo.

jack na jux

Kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV Jux alikiri wazi kuwa alikuwa akitoka kimapenzi na Jackie Cliff na kusema alikuwa anampenda sana licha ya bidada huyo kumzidi umri.

Jux alidai katika kipindi chote ambacho wapo katika mahusiano hakuwahi kutambua wala kuhisi kama Jackie Cliff alikuwa akijihusisha na biashara ya dawa za kulevya mpaka siku alipopata taarifa kuwa amekamatwa ndipo alipojua suala hilo.

“Kiukweli nilimpenda sana Jackie Cliff maana mara nyingi mimi napokuwa na mtu huwa napenda kweli sababu huwa nahitaji kutulia, lakini huwezi amini sikuwahi kutambua kama Jackie Cliff anafanya mambo hayo mpaka alipopata matatizo hayo ndiyo najua mimi, hivyo ilinipa wakati mgumu sana mimi kiasi kwamba nilikuwa sijielewi”. Alisema Jux

Jux aliendelea kudai kuwa wakati Jackie Cliff anapata matatizo hayo yeye alikuwa amekuja likizo Tanzania hivyo ndiyo siku hiyo hiyo ‘Producer’ wake Manecky alipompigia simu na kumwambia aende studio na kumwambia anapaswa kufanya kitu ndipo hapo alianza kuandika na kufanya wimbo wa ‘Nitasubiri’ ambao anadai walishirikiana na watu wengine studio kuutengeneza na kuandika baadhi ya mashairi kwenye wimbo ule ambao ulikuwa maalum kwake.

“Huwezi amini siku ambayo Jackie alipata matatizo Manecky alinipigia simu na kuniambia njoo studio, nilipofika pale akaniambia lazima tufanye kitu ndiyo tukaanza kuandika na kutengeneza wimbo ule, lakini ikitokea ametoka saizi Jackie Cliff sitaweza kuwa naye tena sababu tayari nishaanza maisha mapya” alidai Jux

Eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364