-->

Nimesahau Habari za Shilole- Nuh Mziwanda

Msanii Nuh Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Jike Shupa’ amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye alishasahau habari za Shilole hivyo hata wimbo wake huo mpya hajamuimbia Shilole

nuh-mziwanda

Kama ambavyo baadhi ya watu walikuwa wakihisi kutokana na ujumbe uliopo kwenye wimbo huo.

Nuh Mziwanda akizungumza na eNEWS alisema yeye hawezi kumuimbia mtu mmoja wimbo na kudai kuwa yeye ameimba wimbo wa mapenzi ambao anajua utawagusa watu wengi ambao wamewahi kuumizwa na mapenzi na kuweka sawa kuwa yeye hajaimba wimbo huo kwa ajili ya Shilole.

“Mimi nilishasahau kabisa mambo ya Shilole na huu wimbo sijaimba kwa ajili yake bali nimeimba wimbo kwa ajili ya watu wangu lakini pia hata jina la wimbo huu amelitoa Alikiba mwenyewe baada ya kuimba Chorus” alisema Nuh Mziwanda.

Mbali na hilo msanii huyo ameonyesha kujutia yeye kuvuma zaidi kwa mikasa ya mapenzi kipindi cha nyuma na kudai kuwa ndiyo maana watu walikuwa hawawezi kumsikia sababu alikuwa na kiki nyingi za mapenzi ambazo pia anadai hazijamsaidia kitu chochote kile.

“Unajua ule ni kama utoto ndiyo maana saizi watu walikuwa hawanisikii sababu nilikuwa navuma zaidi kwa kiki za mapenzi na si nyimbo hivyo sikuwa na wimbo kwa sasa ndiyo maana ila kwa sasa watanisikia sababu nataka watu wanisikie kwenye muziki na si mapenzi tena, unajua hata hapa katikati nilijichanganya kidogo baada ya kuanza kumuweka mpenzi wangu kwenye mitandao lakini nilivyoona anaanza kuwa maarufu nilimtoa kwenye mitandao hivyo sasa hivi wala hayuko huko tena” alimalizia Nuh Mziwanda.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364