-->

Nimegundua Mabinti Wanashindwa Kutofautisha Mume na Boyfriend-JB

jb61

Nakaribia 50 sasa na huku mtaani kwetu nimepewa heshima ya mzee wa mtaa… na kila j2 jioni huwa nasuluhisha kesi za wana ndoa…katika kesi nyingi nimegundua mabinti wanashindwa kutofautisha mume na mwanaume wa starehe (boyfriend) na ndio maana una weza ukaenda harusini watu wakabeza aiii kampendea nn??? Anamefata hela tuu…sababu kuna vitu mnaviangalia ambavyo si sifa za mume…ni ziada tu ambayo kama itakuwepo una bahati…mume anatakiwa awe na sifa nyingi lakini kuu ni kuwa macho…masikio…mikono na moyo wake utakuwa kwa mke wake bila kujali wanawake wangapi wazuri wanamwinda…na yuko tayarikuihudumia na kuingalia familia yake…sio lazima awe giant na hb kama jb…wanawake wengi wameishia kuzalishwa na kuachwa na kutengeneza watoto wengi wasio na malezi ya baba na mama…na hawa walioachwa ss wana chuki kubwa na wanaume….pia kizazi hiki cha kuanzia miaka 30 kwenda chini kina wanawake wengi wajeuri wenye kujiamini kupita kiasi…nionavyo huko mbele ndoa zitakuwa chache…wacha nile pilau yangu nijiandae saa 10…kuna wengine wanakuja washatibuana karibia wiki3 sasa

By Jb on Instagram

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364