Mtoto wa Kajala Akerwa na Kazi ya Mama Yake
MTOTO wa muigizaji wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja aitwaye Paula, ametoa mpya baada ya kudai kuwa havutiwi na sanaa anayofanya mama yake, isipokuwa anapenda zaidi uanamitindo.
Akizungumza na gazeti hili, mtoto huyo alisema anavutiwa zaidi na Hamisa Mobeto, ambaye licha ya kuigiza, lakini anatumia sehemu kubwa ya muda wake kufanya uanamitindo, kitu ambacho ni ndoto yake.
“Mimi sijawahi kuvutiwa na kucheza filamu kama mama bali navutiwa na Hamisa Mobeto ambaye anaigiza kidogo sana, mara nyingi anafanya uanamitindo na mimi baadaye nitafuata nyayo yake,” alisema.
Chanzo: GPL