-->

Nina Mchango kwa Vanessa Mdee- Ommy Dimpoz

Ommy amefunguka hayo katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na kituo cha EATV ambapo ameweka bayana kwamba kwa jinsi alivyomfahamu Vanesa Mdee ni mtu wa Kimataifa siku nyingi kwa maana alivyofanya naye huo wimbo alikuwa kwenye ‘media’ kubwa ila alikuwa hajapata pa kutokea tuu.

OMMY687

”Nilipomshirikisha kwenye wimbo wa ‘Me and You’ ikawa kama ni gari limekwama kitonga likawa linasubiri mtu wa kulisukuma na kusonga mbele”.Amesema Ommy.

Msanii huyo amesema anafurahi sana kuona msanii huyo anazidi kuchanja mbuga ikizingatiwa kwamba wasanii wa kike bado siyo wengi nchini, huku akiweka bayana kuwa kufanya matamasha nje ya nchi kwa wasanii wa ndani kunasaidia sana kupata kipato kikubwa kama tamasha likiandaliwa vizuri.

”Ukienda nje unakuta kuna kumbi ambazo ni za waafrika hivyo ukifika kule ukipiga ngoma unakuta watu walishaisikia ndiyo maana ukifanya vizuri ‘kujibrand’ inakuwa rahisi kupata nafasi ya kufanya vizuri nje ya nchi.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364