Ommy Clayton Amleta Gabo na Kitu
MTAYARISHAJI na mtunzi mahiri wa filamu za Kibongo Omary Clayton ‘ Ommy Clayton’ wiki ijayo anatarajia kuachia filamu yake kali nay a kusisimua ya Kitu ambayo amewashirikisha wasanii wakali kama vile Ahmed Salim ‘Gabo’ na wengine.
“Safari hii nimejipanga zaidi kikazi kwani filamu yangu ya Kitu si mchezo unakutana na msanii Gabo kafanya maajabu humo, nafikiri hii itakuwa zaidi ya Ndugu wa mume ni kazi nzuri sana,”anasema Ommy Clayton.
Filamu ya Kitu inasambazwa na kampuni ya Splash Entertainment na kuongozwa na Ommy Clayton wasanii wengine walifanya kazi iwe kazi ni Hemed Suleiman ‘Phd’, Bi. Fety, Hanifa na wasanii wengine wakali kibao wameitendea haki si ya kuikosa.