-->

Ningemkuta mama Kanumba nisingemfukuza-Lulu

Msanii wa filamu Tanzania, Elizabeth Michael alimaarufu kama ‘Lulu’ amefunguka na kusema kuwa yeye hafahamu sababu zilizofanya mama mzazi wa Kanumba asitokee kwenye mapokezi yake baada ya kushinda tuzo nchini Nigeria.

Lulu

Mtangazaji wa kipindi cha eNEWS alihoji ni sababu zipi zimepelekea Mama Kanumba kushindwa kutokea kwenye mapokezi yake ili hali Mama huyo alishiriki kwenye movie hiyo ambayo imempa ushindi Lulu Michael, ndipo hapo Lulu alipodai yeye hatambui sababu na kusema yeye alikuwa Nigeria na watu wote Tanzania walipata taarifa kupitia vyombo vya habari na ndio maana waliweza fika uwanja wa ndege kumpokea hivyo alidai hata kama angemkuta Mama Kanumba hapo ( Uwanja wa ndege) asingeweza kumfukuza.

Kauli hii ya Lulu Michael ni wazi inaonyesha huenda labda hawako sawa na mama mzazi wa Kanumba.

Katika hatua nyingine Baba Mzazi wa msanii huyo alifunguka ya moyoni na kusema kwamba yeye toka awali hakupenda mwanae ajihusishe na masuala ya filamu yeye alitaka mwanae asome shule, lakini anadai kutokana na mafanikio ambayo mwanae ameyapata anaamini kuwa kweli alikuwa amepangiwa kufanikiwa kupitia filamu.

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364