Nipo Kwenye Mahusiano Salama -Mwasiti
Msanii wa bongo fleva hapa nchini Mwasiti Almasi amesema kwamba muonekano wake kwa sasa ni kutokana na kwamba yupo kwenye mahusiano ambayo ni salama.
Mwasiti ametoa ya moyoni alipokuwa akizungumza na EATV kuhusiana na mwonekano wake kwa sasa kuonekana anavutia zaidi tofauti na siku za nyuma.
”Muonekano wangu kwa sasa nina mapenzi ambayo ni salama japo siwezi kumtaja kwa sasa kwa sababu bado ni mapya ila nina faraja sana”
Pamoja na hayo Mwasiti amesema kwamba aina za vyakula kama ugali na dagaa na kupumzika sana hinachangia pia muonekano wake huo.
eatv.tv