-->

Nora Adaiwa Kuwa Chizi Tena!

NURU Nassoro ‘Nora’ ambaye ni mwigizaji wa kitambo Bongo,anadaiwa kuugua uchizi kwa mara nyingine tena, jambo ambalo amelipinga vikali na kwamba wabaya wake wameendelea kumtakia mabaya katika maisha yake, lakini yuko safi na anaendelea na maisha yake.

Nora Katika Pozi

Nora Katika Pozi

Mwanzoni mwa wiki hii, mmoja wa rafiki zake wa karibu aliliambia gazeti hili kuwa, uzushi na uvumi huo ulianza kuenezwa wiki mbili zilizopita, hali iliyosababisha watu wengi, kuanza kumtumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS),wakitaka kuthibitisha uvumi huo, hali iliyomuumiza msanii huyo.

Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora kupitia simu yake ya mkononi ambapo alikiri kukumbwa kukutana na madai hayo huku akionesha masikitiko makubwa juu ya uvumi huo.

NORA788

“Mwenyewe nilishangaa sana, nilishindwa kujua ni kwa nini watu wanaendelea kunitakia mabaya kiasi hiki, nilianza kupokea simu kutoka kwa watu wangu wa karibu wakiniuliza kulikoni, lakini mbaya zaidi nimesikia wanaonizushia na kunitangazia mabaya hayo, baadhi yao ni wasanii wenzangu,” alisema Nora ambaye miaka kadhaa iliyopita aliwahi kudaiwa kuwa chizi.

GPL

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364