-->

Ommy Amjibu Ney Baada ya Kuambiwa ‘Jogoo Hawiki’

Msanii Ommy Dimpoz amejibu mapigo kwa Ney wa Mitego baada ya kumuimba kwenye wimbo wake, huku akimtuhumu eti rafiki zake hawamjui shemeji yao au huenda jogoo hawiki.

ommy632

Ommy Dimpoz amefunguka juu ya hilo na kumrushia makombora ya kutosha Ney wa Mitego, kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa instagram na kuiita barua ya wazi kwa Neema wa Mitego.

“Barua ya wazi kwa Neema wa Mitego kwanza pole kwa malezi ya watoto ambao mama zao wamekukimbia, hakuna mwanamke ambae anaweza kuishi na mwanaume mwenye tabia za kike kama zako? inatakiwa ujiulize una tatizo gani maana kama umaarufu mavi unao, nyumba unayo, magari unayo na hivyo ndo vitu dada zetu wanapenda lakini kwa nini wanakukimbia pili kila nikiwaangalia watoto, naona kabisa hamjafanana kuna umuhimu wa DNA, da Neema trust me”, aliandika Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz aliendelea kumshushia makavu Ney wa Mitego na kusema kuwa yeye na Ney levo zao hazifanani, na kwamba amemjibu ili kuzidi kumpa promo angalau apande chati.

“Hiyo video nimekuwekea hapo juu ni kukuonyesha kuwa mimi na wewe ligi zetu hazifanani, vitu navyokula mimi wewe utaishia kuviona kwenye TV maana kuvipata mpaka uwe unapanda sana Ndege sasa mimi najaza passport ya tatu wakati wewe hata kurasa 4 za passport yako ya kwanza hujamaliza, sasa wewe ushazoea wanawake zako wa jumuiya basi unataka kila mtu apost demu wake, haya sasa chuma hiko kimetoka Ulaya kuja kufuata dodoki”.

“Nimekujibu ili nikusaidie promo ya nyimbo yako atleast upige na vishoo baba, sema nakuomba usirushe ngumi tu maana nakujua mzee wa kupanic maana katika hao mabebi mama wako kuna mmoja nilishapitaga nae, uliza vizuri atakwambia kama jogoo anawika au vipi”, alimalizia Ommy Dimpoz

Eatv.tv

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364