Pasha Amuumbua Snura, Afunguka Haya
Baada ya msanii wa Bongo fleva Snura Mushi kufunguka kuwa hajawahi na hafikirii kutoka na msanii wa Bongo Fleva Pasha amuumbua.
Akizungumza na Enewz Pasha alisema kuwa yeye alishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Snura ila kipindi hiko Snura alikuwa hajaanza kufahamika na yeye alikuwa akitamba na nyimbo ya ni soo.
“Kusema hajawahi kutoka na star hiyo ni uongo na amedanganya mimi nilikuwa na uhusiano nae tena nakumbuka kipindi kile nilikuwa namuimbiaga nyimbo yangu ya ni soo na ile ya am sorry”,alisema Pasha.