Pete ya Uchumba Siyo Kigezo Kuwa Utaolewa- Wolper
Msanii wa filamu nchini Jackline Wolper amesema kwamba siyo vizuri kuzungumzia masuala ya mchumba kwenye vyombo vya habari au kujitangaza sana kwani mtu unaweza kuishia kwenye kuvishwa pete ya uchumba tuu.
Wolper amefunguka hayo katika kipindi cha Nirvana kinachorushwa na EATV ambapo mtangazaji Deogratius Kithama alitaka kujua kwa undani kuhusu mwanadada huyo mrembo ni nani mchumba wake na yupo wapi kwa sasa.
”Mimi sipendi kuzungumzia masuala ya mahusiano yangu na mchumba wangu kwenye vyombo vya habari kwani huweza kutokea mtu akaishia kwenye ‘engagement ring’ hivyo nitasema nikashaolewa na siyo sasa”- Amesisitiza Wolper.
Aidha mwigizaji huyo ameweka wazi kwamba mchumba aliye naye kwa sasa alianza kumtongoza toka mwaka 2012 akakataa ila mambo yalivyoenda ndivyo sivyo kwa mchumba wa awali ikabidi amsikilize huyu ambaye yupo naye kwa sasa.