Picha: Mchekeshaji Mkono Mkonole Afunga Ndoa Kimya Kimya
Msanii wa vichekesho, Mkono Mkonole, Jumamosi hii amefunga ndoa kimya kimya mkoani Tanga na mwanadada aitwae Sabrina Ally.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Mkono amesema amefunga ndoa kimya kimya kutokana na kifo cha msanii mwenzake, Kinyambe aliyefariki Mkoani Mbeya wiki iliyopita na kuzikwa huko huko.
“Nimefunga ndoa jumamosi hii mkoani Tanga, sema ndoa ilikuwa kimya kimya kutokana na msiba wa msanii mwenzetu Kinyambe, lakini nashukuru mungu kila kitu kimeenda sawa,” alisema Mkonole.
Pia Mkonole amesema ameamua kuoa mke ambaye anatoka nje ya tasnia yake ya filamu kwa madai wanawake wa kwenye tasnia hiyo ni wajanja wajanja.
Bongo5