-->

Picha: Young D Akwidwa, Atiwa Mbaroni

Kimemnukia! Mbongo Fleva, David Genzi ‘Young D’ amejikuta mikononi mwa askari wa Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo jijini Dar madai yakiwa kuharibu simu na kushambulia mwili, Amani lina kila kitu.

young-d34

David Genzi ‘Young D’ akiwa amekwidwa

Ilidaiwa kuwa, katika siku za karibuni, msanii huyo alimshambulia mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Nasra lakini pia aliharibu simu yake yenye thamani ya shilingi 600,000.

Juni 6, mwaka huu, yaani Jumatatu iliyopita, Young D akiwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini hapa, aligongewa mlango na kutakiwa kutoka.

young-d1

Lakini alipotoka na kugundua ni askari na wanamtaka waende naye kituoni, alileta ujeuri kidogo, ikabidi wamkwide na kumuweka chini ya ulinzi mpaka kituoni.

“Mbaya zaidi, alikuwa hajavaa shati ni suruali tu, ikabidi aende polisi hivyohivyo. Unajua hawa wasanii wetu bwana sijui huwa wanawaza kitu gani katika ustaa wao,” kilisema chanzo kimoja kilichoshuhudia dogo huyo akiwekwa mtu kati na askari hao.

young-d9

Habari zaidi zinasema kuwa, Nasra na Young D ni wapangaji wa nyumba moja lakini hawana uhusiano mzuri kwani mara kwa mara wamekuwa wakikwaruzana kwa sababu ambazo hazijulikani kirahisi.

“Siku ya tukio, inasadikiwa kuwa walikwaruzana sana, ndipo dogo (Young D) akaamua kumvaa mwanadada huyo na kumpa vitasa (ngumi) kisha kuivunja simu yake,” kiliongeza chanzo.

young-d

Katika Wabongo Fleva wanaotamba, Young D naye yumo ambapo amepata jina kupitia vibao vyake viwili, Ujanjaujanja na Kijukuu.

Askari mmoja wa Kituo cha Urafiki ambaye aliomba asiandikwe jina kwa sababu si msemaji, alipoulizwa na Amani kuhusu hatima ya mwimbaji huyo alisema: “Upelelezi unaendelea, ukikamilika atapelekwa mahakamani.”

Chanzo: GPL

 

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364