-->

Rich Mavoko:Kuna Msanii Mkubwa Alinikataza Kwenda Wasafi, Alimjibu Hivi

Msanii Rich Mavoko ambaye sasa yupo chini ya Label ya WCB Wasafi amefunguka na kusema kuwa wakati tetesi za yeye kwenda kujiunga na label ya WCB Wasafi zimeenea kuna msanii mmoja mkubwa wa bongo fleva alimtumia ujumbe na kumwambia anaanzaje kwenda kusimamiwa kazi na msanii Diamond Platnum.

RICH MAVOKO

Rich Mavoko

Rich Mavoko amesema hayo leo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana kwa maneno yake hayo ila yeye ilibidi amjibu tu kuwa yeye hafamu ametoka wapi na anakwenda wapi hivyo hawezi kujua mipango ya Mungu kwenye safari yake ya muziki.

“Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu” alisema Rich Mavoko.

eatv.tv

NUNUA FILAMU KUTOKA STEPS ENTERTAINMENT: TUNAKUFIKISHIA POPOTE PALE ULIPO:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

KAMA UNATAKA KUWA WAKALA WA KUSAMBAZA FILAMU POPOTE PALE:

Piga namba hizi: 0673 348 364 au 0754 256 489.

Filamu Zilizotoka Hivi Sasa >>>>HIZI HAPA

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364