-->

Monalisa Aliamsha Tuzo za Kimataifa

MWIGIZAJI mwenye mvuto nchini, Yvonne Cherryl ‘Monalisa’, amechaguliwa katika kinyang’anyiro cha tuzo zinazojulikana kwa jina la The African Prestigious Awards akigombea kama mwigizaji Nyota wa Kike wa Mwaka.

Washindi wa tuzo hizo hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki na Monalisa amewaomba mashabiki wake kutomwangusha.

“Ninawaomba mashabiki wangu wote kwa jumla kunipigia kura ili niweze kubeba tuzo. Ni rahisi tu, mtu anaingia www.africanprestigiousawards.com/voting na kwa maelezo mengine wachungulie kurasa zao za mitandao ya kijamii,” alisema.

Mwanadada huyo aliyeanza kuigiza tangu enzi za Mambo Hayo, huwa amekuwa na bahati ya kuteuliwa katika tuzo mbalimbali nje ya nchi na alisema anaamini akipigiwa kura za kutosha ataipeperusha bendera ya Tanzania katika anga hizo za kimataifa.

Mwanaspoti

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364